Form 4 Kiswahili Study Notes

HALMASHAURI YA WILAYA YA ITILIMAMTIHANI WA UTIMILIFU KIDATO CHA NNE 021 KISWAHILI

 

Muda: Saa 3
Jumatatu, 13 Julai 2020 asubuhi

 

MAELEKEZO:

  1. Karatasi hii ina sehemu A, B na C zenye jumla ya maswali kumi na mbili (12).
  2. Jibu maswali yote katika sehemu A na B na maswali matatu (3) kutoka sehemu C.
  3. Zingatia maagizo ya kila sehemu na ya kila swali.
  4. Simu za mkononi na vitu vyote visivyoruhusiwa havitakiwi katika chumba cha mtihani.
  5. Andika Namba yako ya Mtihani katika kila kurasa ya kujibia

     

     

 

 

SEHEMU (Alama 15)

Jibu maswali yote katika sehemu hii

 

1. Chagua herufi ya jibu sahihi katika vipengele (i) hadi (x) kisha andika herufi ya jibu hilo katika

karatasi ya kujibia.

 

  1. Zifuatazo ni sifa za lugha isipokuwa

    A lugha huzaliwa B lugha hukua

    C lugha haifi D lugha ni mali ya binadamu

    F lugha ina ubora wake

  2. Shamba letu li kubwa neno “Li” ni aina gani ya neno?
    1. Kiwakilishi
    2. Kielezi
    3. Kivumishi
    4. Kiunganishi
    5. Kitenzi kishirikishi
  3. Lugha fasaha hufuata taratibu zaq lugh, taratibu hizo ni pamoja na

    A fonolojia, mofolojia, semantiki na sintaksia

    B maana, matamshi, muundo na maumbo

    C maana, matamshi, muundo na mantiki

    D kiimbo, shada, mkazo na toni

    F fonolojia, mkazo, shada na semantiki

  4. Kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki (the interteritorial Swahili language committee) iliteua lahaja moja na kuisanifisha, lahaja hiyo ilikuwa ni

    A kimvita B kiunguja

    C kimtang’ata D kisiu

    F kivumba

  5. Watoto hawa wanacheza vizuri neno “Vizuri” ni aina gani ya neno?
    1. Kivumishi
    2. Kielezi
    3. Kiwakilishi
    4. Kivumishi cha sifa
    5. Kihisishi

       

  6. Kiswahili ni kibantu kwa kuwa:-
    1. Kinaongewa na wabantu wengi
    2. Ni lugha ya Taifa
    3. Kina maneno mengi ya kibantu
    4. Kimethibitishwa kiisimu na kihistoria
    5. Wasomi wengi wamethibitisha hivyo.
  7. Ni jambo gani linalodhihirisha upekee wa kazi fuani ya kifasihi?
    1. Muundo
    2. Mtindo
    3. Wahusika
    4. Jina la mtunzi
    5. Jina la kazi husika

 

 

 

  1. Ipi ni fasili sahihi kuhusu tungo?
    1. Maneno yanayoonesha uhusiano baina ya neno moja na jingine.
    2. Kipashio kidogo katika lugha kinachotumika kama dhana ya kuchambulia lugha Fulani.
    3. Matokeo ya kuweka na kupanga pamoja vipashio sahili ili kujenga vipashio vikubwa zaidi.
    4. Kipashi cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea
    5. Maneno yenye kutoa maana kamili
  2. Nini maana ya sentensi sahili.
    1. Ni sentensi yenye kishazi huu kimoja au zaidi pamoja na kishazi tegemezi.
    2. Ni sentensi yenye kishazi huru
    3. Ni sentensi yenye kuonesha masharti
    4. Ni sentensi yenye maana nyingi
    5. Ni sentensi yenye vishazi vingi
  3. Zifuatazo ni sifa za pijini isipokuwa

    A. Pijini huwa na maneno kutoka lugha mbili au zaidi

    B. Pijini hutokea kurahisisha mawasiliano baina ya watu ambao kila mmoja

    ana lugha yake

    C. Miundo ya maneno na tungo katika pijini imerahisishwa ili kukidhi

    mawasiliano

    D. Pijini haina msamiati mwa kutosha, hivyo wazungumzaji hutumia sana

    ishara

    1. Pijini ina watu ambao kwao hiyo ni lugha yao ya kwanza

 

2. Oanisha maana za dhana za uandishi zilizo katika orodha A kwa kuchagua herufi ya dhana

husika katika orodha B kisha andika herufi husika katika orodha B kisha andika herufi husika

katika karatasi ya kujibia.

 

Orodha A

Orodha B

  1. Sehemu ya neno inayobakia baada ya kuondolea aina zote za viambishi.
  2. Hujengwa na mzizi asilia pamoja na viambishi tamati vijenzi
  3. Mzizi unaobakia baada ya kuondondewa viambishi tamati maana.
  4. Mzizi wowote yaani mzizi asilia au mzizi wa mnyumbuliko
  5. Sehemu ya neno ambayo huweza kutamkwa mara moja na kwa pamoja kama fungu la sauti
  1. Mzizi asilia
  2. Irabu
  3. Mzizi/ kiini
  4. Silabi
  5. Mzizi wa mnyumbuliko
  6. Shina la kitenzi
  7. Mzizi asilia maana
  8. Kitenzi
  9. Mnyumbuliko
  10. Uambishaji

 

 

SEHEMU B (Alama 40)

Jibu maswali yote katika sehemu hii.

 

  1. (a) Onesha mizizi ya maneno yafuatayo kwa kupigia mstari mizizi hiyo

    (i) Salisha

    (ii) Anakunywa

    (iii) Wamekula

    (iv) Onesha

    (b) Taja aina za maneno yaliyopigiwa mstari katika sentensi zifuatazo. Usitumie msimbo,

    mfano kama ni kiwakilishi usiandike “W”, andika “Kiwakilishi”.

(i) Bata maji anaogelea vizuri.

(ii) Kucheza tunakupenda ingawa kunapoteza muda.

(iii) Kijana ndiye msomaji hodari.

(iv) Mwl. J. K.Nyerere alikuwa rais bora Afrika.

 

  1. Istilahi moja inaweza ikawa na majina mawili. Andika jina jingine kwa kila moja ya dhana zifuatazo.
    1. Sentensi huru
    2. Kitenzi kikuu
    3. Kirai nomino
    4. Kitamkwa cha msingi

       

  2. Eleza njia nne (4) za uundaji wa maneno ya Kiswahili kwa kutoa mfano mmoja kwa kila njia.
  3. Kamati ya lugha ya Afrika ya Mashariki iliyoundwa 1930 ilikuwa kama moto wa ndaamba katika kuimarisha matumizi ya Kiswahili Afrika ya Mashariki. Jadili kauli hii kwa kutumia hoja nne (4).
  4. Kwa kutumia mifano minne (4) eleza jinsi matumizi ya viungo vya mwili yanavyokamilisha fasihi simulizi.
  5. Soma kifungu cha habari kifuatacho, kisha jibu maswali yanayofuata.

    Hawa jamaawalirithi. Walirithi hawa jamaa. Walirithi. Walirithi. Jamaa waligawana vitu.walirithi kila kitu kilichokuwa ndani ya nyumba. Walirithi michungwa na miembe. Walirithi migomba yote. Walirithi paka nambwa. Walirithi majani yaliyokuwa juu ya paa, na miti yote iliyofanya nyumba isimame. Walirithi mashamba yote. Walirithi kuku; walirithi hata mbolea ya ng’ombe. Walirithi. Hawa jamaa, kweli walirithi. Lakini hapakuwa hata na mtu mmoja aliyeweza kusema atamchukua mtoto Fulani amtunze. Badala yake walimdai Mabula alipe mahari ili pia wagawane. Vitu vya Misana vilikwenda kuchukuliwa.

    Baada ya kugawana vitu hivi, watoto walikaa pale nyumbani kwa muda wa siku moja tu. Kila kitu walichogusa waliambiwa sio chao, “Pesa zenu zimo benki”, walitulizwa. Midala aliwaomba Masista waliokuwa wakikaa Kilulu wamsaidie kutunza dada zake kwa muda wa miaka miwili. Hawakukataa: walimuonea huruma. Baada ya siku moja, Stela, Nkamba na Emma walipelekwa huko. Midala alifunga safari kurudi Kahama pamoja na Mabula. Maafa yalimfanya Mabula ampende zaidiu Midala. Huruma iliwafanya kweli wapendane. Wakiwa bado nyumbani, Mabula alimkumbatia Midala na kumwambia: ‘Midala mimi nitakutunza; baada ya muda wa miaka miwili ya kazi, nitawatunza wadogo zako’.

    Midala aliwaambia wale watu waliojida jamaa zake; “Mabula hatatoa hata chapa kwa ajili yenu. Kuwatunza wadogo zangu- hakuna mahari ipitayo hiyo”. Walifunga safari mpaka Kahama. Waliishi kama mme na mke. Huko nyuma jamaa zake waliangusha nyumba na kutoa majani pamoja na miti. Wakagawana.

    Maswali

    1. Pendekeza kichwa cha habari hii kisichozidi maneno matatu.
    2. Unafikiri kwa nini Midala alikataa asitolewe mahari na Mabula?
    3. Mwandishi wa habari hii anaichukuliaje jamii ya akina Midala?
    4. Kutokana na habari uliyiosoma, eleza matatizo mawili yanayowakabili yatima pindi wazazi wao wote wanapoaga dunia bila kuacha urithi kwa watoto wao.

       

      SEHEMU C (Alama 45)

          Jibu maswali matatu (3) katika sehemu hii

       

9. a) Eleza mambo matatu (3) muhimu ya kuzingatia wakati wa uandishi wa barua za simu.

b) Umechaguliwa kujiunga na elimu ya upili wa juu katika Shule ya Sekondari Magufuli

iliyoko wilayani Chato S.L.P 21. Muandikie barua ya simu baba yako ukimtaarifu kuwa

umeishiwa; sabuni, kalamu, daftari na mafuta ya kujipaka. Tumia maneno kumi (10) tu.

Jina lako ni Kija Madonange, baba yako anaitwa Mashilingi Michembe wa Laini,

S.L.P 12 Bariadi.

    

ORODHA YA VITABU KWA SWALI LA 10 – 12

 

USHAIRI

  • Wasakatonge      – M.S KHATIBU (D.U.P)
  • Malenga wapya      – TAKILUKI (D.U.P)
  • Mashairi ya chekacheka – T.A MVUNGI (EP&D LTD)

RIWAYA

  • Takadini      – BEN J. HANSON (MBS)
  • Watoto wa mamantilie     – E. MBOGA (HP)
  • Joka la mdimu      – A. J SAFARI (HP)

TAMTHILIYA

  • Orodha      – STEVE REYNOLDS (MA)
  • Ngoswe penzi kitovu cha uzembe – E. SEMZABA (ESC)
  • Kilio chetu      – MEDICAL AID FOUNDATION (TPH)    
  1. Jadili jinsi gani majina ya riwaya za “Joka la Mdimu” na “Watoto wa Mama N’tilie” yanavyosadifu maudhui ya riwaya hizo. Toa hoja tatu toka katika kila riwaya.
  2. Washairi hutoa mashairi yenye mafunzo kwa jamii zao. Thibitisha hoja hii kwa kutumia diwani mbili ulizosoma.

12. Kwa kutumia tamthiliya mbili ulizosoma, fafanua madhara yanayotokana na

kukosekana kwa elimu ya jinsia kwa vijana kwa kutoa hoja tatu kutoka katika kila

kitabu.

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.